Our Services

Explore our comprehensive range of professional wellness services.

60 min

UZITO RESET 90™ – Huduma ya Usimamizi Binafsi wa Kupunguza Uzito, Kitambi & Nyama Uzembe

MAELEZO YA HUDUMA


UZITO RESET 90™

UZITO RESET 90™ ni programu ya siku 90 ya usimamizi wa karibu kila siku inayolenga:

  • Kuondoa uzito mkubwa
  • Kupunguza kitambi
  • Kuimarisha umbo (nyama uzembe)


Hii si dawa ya miujiza, bali ni mfumo unaofanya kazi unaozingatia:

  • Hali halisi ya afya yako
  • Ratiba yako ya maisha
  • Malengo yako binafsi


Unasimamiwa hatua kwa hatua mpaka uone mabadiliko ya kweli.


UNACHOPATA (FAIDA KUU)

Usimamizi wa kila siku kwa siku 90 – hauko peke yako kwenye safari

Ushauri binafsi (1:1) kulingana na afya, umri, jinsia na ratiba yako

Mpango wa lishe uliobinafsishwa (vyakula vya Kitanzania vinavyopatikana kirahisi)

Ujumbe wa ukumbusho & motisha kila siku

Mwongozo wa maji, muda sahihi wa kula & mbinu za kuchoma mafuta

Ufuatiliaji wa maendeleo (uzito, tumbo, mabadiliko ya mwili)

Elimu ya tabia za kula ili matokeo yadumu muda mrefu

Marekebisho ya mpango pale inapohitajika endapo afya au mazingira yatabadilika


INAWALENGA NANI?

✔ Wenye uzito mkubwa au kitambi sugu

✔ Waliokata tamaa baada ya kujaribu njia nyingi bila mafanikio

✔ Wanaotaka mabadiliko ya kweli, si ya muda mfupi

✔ Wanaohitaji msimamizi wa karibu ili wabaki kwenye mpango


MATOKEO UNAYOTARAJIA

🔥 Kupungua kwa uzito & kitambi kwa njia salama

💪 Kuimarika kwa umbo, nguvu na wepesi wa mwili

🧠 Nidhamu ya kula & uelewa wa mwili kuongezeka

♻️ Matokeo ya kudumu, si kurudi nyuma haraka


GHARAMA YA HUDUMA

💰 Tsh 50,000 tu – kwa siku 90 kamili

(Ada hii ni kwa usimamizi wa kila siku, ushauri binafsi, na ufuatiliaji wa maendeleo)


JINSI YA KUJIUNGA

📩 Tuma ujumbe: “UZITO RESET 90”

📲 WhatsApp / Piga simu: 0767 716 093


Anza leo.

Badilisha mwili wako kwa mfumo unaokuelewa, unaokusimamia, na unaokusukuma mpaka uone matokeo.

Price TSH 50,000
60 min

Ushauri wa Afya- Kufika Ofisini Bila Kuchukua Tiba

Huduma hii inalenga mtu anayehitaji tathmini ya kina ya afya yake na mwongozo sahihi wa kuboresha afya na mtindo wa maisha, kwa njia salama, ya kitaalamu na ya faragha.

Ni huduma ya mtu mmoja mmoja, inayozingatia hali halisi ya mwili wako — si ushauri wa jumla.


NDANI YA DAKIKA 60, UNAPATA:

Uchunguzi wa awali wa afya

Ushauri wa kina wa kiafya

Mpango binafsi wa wiki 4 kulingana na mahitaji yako halisi


HUDUMA INAJUMUISHA:

📝 Fomu ya tathmini ya afya & mtindo wa maisha

— historia ya afya, lishe, usingizi, shughuli na changamoto zako


🥗 Mpango wa lishe uliobinafsishwa

— unaoendana na hali ya mwili wako na malengo yako


🏋️ Mwongozo wa mazoezi ya nguvu & uimara

— (strength & endurance) kulingana na uwezo wako


🧠 Ushauri binafsi wa kitaalamu

— kuelewa chanzo cha changamoto zako na hatua sahihi za kuchukua


📲 Follow-up ya karibu kupitia WhatsApp

— kukusaidia kutekeleza mpango kwa usahihi


🎁 Bonus: Video au sample za msaada

— kulingana na mahitaji yako binafsi


MAHALI PA HUDUMA

📍 Okoa Mwili Natura-Ceutical Clinic

Kinondoni, Dar es Salaam


GHARAMA & MALIPO

💰 Tsh 100,000 tu


💳 Malipo yanaweza kufanyika:

✔ Kwa simu

✔ Moja kwa moja ofisini


👉 Jisajili leo na chukua hatua ya kuboresha afya yako ndani ya wiki 4 kwa mwongozo sahihi.


📞 Wasiliana nasi:

+255 767 716 093

Price TSH 100,000
60 min

Online (Ushauri Binafsi Inbox Kwako Kwa Siku 30)

HUDUMA YA USHAURI BINAFSI

(1–ON–1 CONSULTATION)


Huu ni mpango maalum wa mtu mmoja kwa mmoja (1–on–1) unaomlenga mtu anayehitaji msaada wa karibu, wa kina na wa siri kuhusu afya yake, kulingana na hali halisi ya mwili wake.


HUDUMA HII INALENGA:

✔ Afya ya uzazi (mwanaume na mwanamke)

✔ Nguvu za kiume na utendaji wa uzazi

✔ Kupunguza uzito mkubwa & kitambi

✔ Matatizo ya ini

✔ Magonjwa ya figo

✔ Matatizo ya ngozi

✔ Matatizo ya mifupa

✔ Magonjwa ya moyo na mishipa

✔ Utendaji wa mwili na afya kwa ujumla


UNACHOPATA KUPITIA USHAURI HUU

Kupitia mawasiliano ya mtandaoni, unapata:


🧠 Ushauri wa siri na wa faragha (1–on–1)

— bila aibu, bila hukumu, bila shinikizo


💬 Majibu ya kina ya maswali yako yote

— yakizingatia historia yako ya afya, dalili na malengo


🥗 Mpango binafsi wa tiba asili

— juisi, lishe, ratiba na dozi vinavyolingana na mwili wako na changamoto zako


📅 Ufuatiliaji wa siku 30

— kuhakikisha unaelewa mpango, unatekeleza kwa usahihi, na unaanza kuona mabadiliko halisi


LENGO LA HUDUMA

🎯 Huduma hii inalenga kutatua chanzo cha tatizo, si kuficha dalili, kwa kutumia:

✔ Elimu sahihi ya afya

✔ Lishe inayofaa mwili wako

✔ Mabadiliko ya mtindo wa maisha yanayodumu


GHARAMA & UPATIKANAJI

💰 Tsh 50,000 (USD 21) tu kwa siku 30


Nafasi ni chache kwa mwezi – watu 5 tu

(Hii ni kuhakikisha kila mshiriki anapata usimamizi wa kweli na wa karibu)


👉 Ushauri wa kweli huanza kwa kuuelewa mwili wako,

na kuchukua hatua sahihi kwa wakati sahihi.


📲 Wasiliana sasa ili kuhifadhi nafasi yako.

Price TSH 50,000
90 min

Mafunzo Ya Kila Siku Ndani Ya WhatsApp Group

HUDUMA YA ELIMU YA AFYA


BURE KABISA

Huduma hii ya ELIMU YA AFYA (BURE) inamwezesha mtu aliyekomaa kupata mafunzo ya kila siku yanayosaidia kuboresha afya kwa mwanaume na mwanamke kwa njia asili, salama na endelevu, bila kutumia dawa hatarishi au suluhisho za muda mfupi.


Elimu inalenga kujenga uelewa sahihi wa mwili na kufanya mabadiliko ya kweli ya kiafya kupitia maarifa.


HUDUMA HII INALENGA:

✔ Afya ya uzazi (mwanaume na mwanamke)

✔ Kupunguza uzito mkubwa, kitambi & nyama uzembe

✔ Afya ya mifupa, moyo, ini na figo

✔ Matatizo ya ngozi

✔ Lishe sahihi na mtindo bora wa maisha


UNACHOJIFUNZA KUPITIA ELIMU HII

Kupitia elimu rahisi na inayoeleweka, washiriki hujifunza:


FAIDA ZA KUJIUNGA

✅ Kuelewa chanzo halisi cha matatizo ya uzazi, uzito na magonjwa sugu

✅ Kujifunza lishe sahihi ya kila siku kwa afya bora bila kujiumiza

✅ Kupata mbinu za asili za kusaidia usawazishaji wa homoni, nguvu ya mwili na kinga

✅ Kujifunza namna ya kupunguza uzito kwa usalama na kudumisha matokeo

✅ Kusaidia ngozi kujirekebisha kutoka ndani (inner healing)

✅ Kupunguza utegemezi wa dawa zisizo za lazima

✅ Kujenga afya ya muda mrefu, si suluhisho la muda mfupi

✅ Kujitibu kwa maarifa sahihi na kufanya maamuzi bora ya maisha

🎯 Lengo kuu: Mabadiliko ya kweli na endelevu — si tiba za haraka zisizodumu.



👉 Jifunze. Badilika. Jitibu kwa Elimu.

JIUNGE NA MAKUNDI YA ELIMU (BURE)

🧴 Group la Mafunzo ya Ngozi

👇👇

https://chat.whatsapp.com/Lipzy70x4xN93KZO36Ldna?mode=r_c



🤰 Group la Mafunzo ya Uzazi

(Kwa mwanaume na mwanamke)

👇👇

https://chat.whatsapp.com/FyxIL6j4uyCEss8nzxINNn?mode=r_c



⚖️ Group la Kuondoa Uzito, Kitambi & Nyama Uzembe

👇👇

https://chat.whatsapp.com/EaTzNlmpv7yCKo3MUBh738?mode=r_c


Elimu ni msingi wa afya bora.

Jiunge leo – ni bure, lakini thamani yake ni kubwa.

Price TSH 0
60 min

Kupata Miadi (Appointment) Na Daktari Kwa Ushauri Wa Moja Kwa Moja

🩺HUDUMA YA USHAURI WA AWALI (INITIAL CONSULTATION)


Huduma hii humuwezesha mteja kuzungumza moja kwa moja na mtaalamu wa afya (daktari) kwa njia salama na rahisi, kulingana na upatikanaji wake.


📲 Njia za Ushauri:

  • 📞 Simu ya kawaida
  • 🎧 Voice Call (WhatsApp/mtandao)
  • 🎥 Video Call


📞 Mawasiliano ya Huduma:

+255 767 716 093


🧠 Mteja Atapata Nini Katika Ushauri wa Awali?

✅ Kusikilizwa kwa makini kuhusu changamoto yake ya kiafya

✅ Nafasi ya kueleza dalili, historia fupi ya tatizo, na hofu alizonazo

✅ Ushauri wa kitaalamu wa awali (initial medical guidance)

✅ Mwongozo wa hatua sahihi za kuchukua kulingana na hali yake, ikijumuisha:

  • Kufanya vipimo vinavyohitajika
  • Marekebisho ya lishe au mtindo wa maisha
  • Kuandaliwa mpango sahihi wa matibabu au huduma inayofuata


🔒 Faragha na Utaratibu

Huduma hii ni ya faragha kabisa (confidential) na hutolewa kwa mfumo wa miadi, ili kuhakikisha mteja anahudumiwa kwa utulivu, umakini na bila haraka.

Price TSH 15,000